Alhamisi 3 Septemba 2026 - 18:13
Hukumu za Kisheria: Mazungumzo Kabla ya Ndoa na Faragha

Hawza/ Ayatullah Sayyid Ali Sistani amejibu swali la kisheria (istiftaa) kuhusu “mazungumzo kabla ya ndoa na faragha.”

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Sayyid Ali Sistani amejibu swali la kisheria kuhusu “mazungumzo kabla ya ndoa na faragha,” ambalo tunaliwasilisha hapa kwa wasomaji na wale wanaopenda kufahamu hukumu hiyo.

Mazungumzo Kabla ya Ndoa na Faraghs

Swali:
Je, inaruhusiwa kuzungumza na mchumba (mtu anayetarajiwa kufunga naye ndoa, kwa lengo la kufahamiana zaidi)?

Jibu:
Iwapo watazingatia heshima na staha katika kutazamana na kuzungumza, na wakawa na uhakika wa kujilinda dhidi ya kutumbukia katika dhambi, basi hakuna tatizo kwenye kulifanya hilo.

Hata hivyo, kufanya mzaha wa kimapenzi na kuingia katika mazungumzo yasiyo na maadili au ya kimapenzi ni haramu.

Lakini mambo yote hayo yanakuwa halali baada ya kufungwa ndoa ya kisheria (aqdi ya Sharia).

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha